Ajira

Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal na Utumishi 2025 / 2026 PDF

Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal na Utumishi 2025 / 2026 PDF

Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal na Utumishi 2025 / 2026 PDF Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji wote waliotuma maombi ya kazi katika MDAs na LGAs kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 24 Mei hadi 28 Mei 2025. Baada ya usaili huo, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi.

Waombaji wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo kwa umakini mkubwa:

Maelekezo Muhimu kwa Washiriki wa Usaili

  1. Ratiba ya Usaili:
    Usaili utafanyika kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili. Muda na eneo la usaili vimebainishwa kulingana na kada husika. Hakikisha unafahamu tarehe yako.
  2. Uvaaji wa Barakoa:
    Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa kama sehemu ya tahadhari za kiafya.
  3. Utambulisho Binafsi:
    Wasailiwa wote wanapaswa kuwa na kitambulisho halisi kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni:
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
    • Kitambulisho cha Mpiga Kura
    • Pasipoti (Passport)
    • Leseni ya Udereva
    • Kitambulisho cha kazi
    • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa au Kijiji
  4. Vyeti Halisi vya Elimu:
    Msailiwa anatakiwa kufika na vyeti halisi vya:
    • Cheti cha kuzaliwaKidato cha Nne (IV) na Sita (VI)Diploma (Astashahada/Stashahada)Stashahada ya Juu, Shahada au zaidi (kutegemeana na sifa alizoomba nazo)
    Vyeti visivyokubalika ni pamoja na:
    • Testimonials
    • Provisional Results
    • Statement of Results
    • Result slips za Form IV na VI
      Wasailiwa wenye nyaraka hizi hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
  5. Gharama za Usaili:
    Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi wakati wote wa usaili.
  6. Taarifa Sahihi za Usaili:
    Hakikisha unazingatia tarehe, muda na eneo ulilopangiwa. Kukosekana kwa muda ni sababu ya kuenguliwa.
  7. Uhakiki wa Vyeti kwa Waliosoma Nje:
    Waombaji waliohitimu nje ya Tanzania wanapaswa kuwa na vyeti vilivyohakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTVET au NECTA.
  8. Leseni na Usajili kwa Kada Maalum:
    Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuwasilisha vyeti vya usajili halisi pamoja na leseni za kazi.
  9. Namba ya Mtihani:
    Wasailiwa wote wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kunakili namba ya mtihani, kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
  10. Tofauti ya Majina:
    Kwa wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana kwenye nyaraka mbalimbali, wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
  11. Waombaji Wasioitwa:
    Waombaji ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili, wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kuona sababu za kutokuitwa na kujiandaa vyema kwa nafasi zijazo.

Pakua orodha ya kuitwa kwenye usaili Ajira portal na Utumishi hapa

Soma zaidi: Ajira Mpya Mkapa Foundation, TAESA Nafasi za Kazi 800

1 Comment

Leave a Comment