Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Ajira portal Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 22/06/2025 hadi tarehe 23/06/2025. Baada ya usaili, waombaji kazi watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi.
Maelezo muhimu kwa wasailiwa:
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Muda na sehemu ya kufanyia usaili zimeainishwa kwa kila kada husika.
- Kila msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Wasailiwa wote wanapaswa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Cheti cha Kidato cha IV
- Cheti cha Kidato cha VI
- Stashahada
- Stashahada ya Juu
- Shahada ya Kwanza au zaidi (kutegemeana na sifa za Mwombaji)
- Hati zifuatazo hazitakubaliwa na msailiwa hataruhusiwa kuendelea na usaili:
- Testimonials
- Provisional Results
- Statement of Results
- Form IV na Form VI Results Slips (hati za matokeo)
- Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri, na malazi.
- Wasailiwa wanapaswa kuzingatia tarehe, muda, na mahali walipopangiwa kufanyia usaili.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya Tanzania watahakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama vile TCU, NACTE au NECTA.
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pale nafasi zitakapotangazwa tena, kwa kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanatakiwa kuja na:
- Vyeti halisi vya usajili
- Leseni halisi ya kufanyia kazi
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili watahakikisha wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani, kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
Pakua PDF hapo chini.
GIPHY App Key not set. Please check settings