TAESA, Kujisajili na Kutuma Maombi ya Ajira 2025 / 2026 Tanzania Employment Services Agency (TAESA) ni wakala wa serikali unaosaidia watanzania kupata ajira kwa kuwaunganisha na waajiri wa ndani na nje ya nchi. TAESA pia hutoa mafunzo ya kujiandaa kwa soko la ajira.
Huduma Kuu za TAESA
- Ushauri wa ajira
- Mafunzo ya uandishi wa CV na usaili
- Kuunganisha waajiri na waombaji
Kwa Mlioko Mbali na Ofisi Za TAESA Mnaweza Kutuma Maombi Kupitia Email.
Email: info@taesa.go.tz
Kujisajili tembelea kwenye tovuti yao ambayo ni https://jobs.kazi.go.tz.
Jinsi ya kujisajili TAESA
Kujisajili na Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Ajira (Employment Management Information System) umetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha mwingiliano rahisi na vipengele mbalimbali kama vile:
- Uundaji wa Akaunti
- Upatikanaji wa Mfumo
- Usajili
- Usimamizi wa Mipaka ya Ajira.

Uundaji wa Akaunti
- Fungua kivinjari (browser) kisha andika anwani: jobs.kazi.go.tz kwenye mstari wa anwani (address bar).
- Bonyeza Enter kufungua ukurasa wa kuingia kwenye mfumo.
- Bofya Login.
- Bofya Create Account.
- Jaza taarifa zote zinazohitajika.
- Bofya Create Account kukamilisha.
- Nenda kwenye barua pepe yako ili kuthibitisha na kuamilisha akaunti yako.
Usajili kwa Watafuta Ajira
Chagua Aina ya Akaunti:
- Ingia kwenye mfumo kwa kutumia akaunti yako.
- Chagua Jobseeker kama aina ya akaunti.
- Bofya Proceed ili kuendelea.
Hakiki Namba ya NIDA na Jaza Taarifa Msingi
- Weka Namba yako ya NIDA.
- Bofya Verify NIDA kisha jibu maswali ya uthibitisho kwa usahihi.
- Baada ya uthibitisho kufanikiwa, jaza taarifa zote muhimu kama mtafuta ajira.
Soma zaidi: Wizara ya Afya, Ajira kwa Wataalamu wa Afya 2025 / 2026