Nafasi za Kazi Afisa Kumbukumbu Daraja II MDAs & LGAs Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha Maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi (10) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Nafasi: Afisa Kumbukumbu Daraja II – Nafasi 10
Mwajiri: Wizara, Idara Zinazojitegemea (MDAs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs)
Muda wa Kutuma Maombi: 05 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025
Muhtasari wa Kazi: Hakuna
Majukumu ya Kazi:
- Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, pamoja na kutunza na kusimamia matumizi ya kumbukumbu katika Wizara, Idara zinazojitegemea, vituo vya kutunzia kumbukumbu, mikoa, manispaa, halmashauri za wilaya, nyaraka za Taifa na mashirika ya umma kulingana na mahali atakapopangiwa.
- Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masjala za Wizara, mikoa, idara zinazojitegemea, manispaa, halmashauri za wilaya na vituo vya kuhifadhia kumbukumbu na nyaraka za Taifa.
- Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa kwa kutumia kompyuta, pamoja na kuzitunza na kusimamia matumizi yake katika Wizara, Idara zinazojitegemea, taasisi na serikali za mitaa kulingana na mahali alipo.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.
Sifa za Mwombaji:
Mwombaji awe na shahada ya kwanza katika fani ya Utunzaji na Uhifadhi wa Kumbukumbu au fani nyingine inayolingana nayo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
Mshahara: Ngazi ya TGS D kwa mujibu wa viwango vya Serikali.
Tuma maombi hapo chini.
GIPHY App Key not set. Please check settings