Ajira

Mwongozo wa Walimu Kujitolea, Fursa za Ajira 2025

Mwongozo wa Walimu Kujitolea, Fursa za Ajira 2025

Mwongozo wa Walimu Kujitolea, Fursa za Ajira 2025 umeandaliwa ili kutoa maelekezo ya namna ya kupata walimu wenye sifa stahiki na kuwaajiri kwa mkataba wa kujitolea, kutoa taratibu za mafunzo kabilishi, kupanga na kutoa maelekezo ya kutosha kitaaluma na kitaalamu ili kazi zifanyike kwa ufanisi. Aidha, Mwongozo huu unalenga kutoa maelekezo ya upatikanaji wa walimu wanaojitolea na huduma zao ikiwaemo: posho, motisha na usimamizi wa nidhamu pahala pa kazi kwa kuzingatia masharti ya ajira za mkataba.

Inatarajiwa kuwa matumizi ya Mwongozo huu yataimarisha ushirikiano wa wadau wa elimu hususani Uongozi wa Elimu, jamii, walimu na wazazi. Pia Mwongozo utawezesha walimu wanaojitolea kutoa huduma stahiki za ujifunzaji na ufundishaji kwa kuzingatia matakwa ya elimu nchini. Hii itasaidia kutatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji na kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa katika elimu ya awali, elimu ya msingi, elimu ya sekondari na vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania.

Malengo Mahususi

i. Kufanya Ualimu wa Kujitolea kuwa kazi yenye makubaliano mahususi kwa mujibu wa Mwongozo huu;

ii. Kuongeza idadi ya walimu wenye sifa stahiki shuleni;

iii. Kusimamia utekelezaji wa majukumu ya kila ngazi inayohusika katika usimamizi wa walimu wa kujitolea;

iv. Kuongeza ufanisi wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji shuleni na katika vyuo vya maendeleo ya wananchi; na

v. Kuhakikisha taratibu na maadili ya kazi ya ualimu yanazingatiwa katika kutumia huduma ya walimu wa kujitolea.

Vigezo vya Walimu Kujitolea

Ili kuwa mwalimu wa kujitolea, mtu anatakiwa kuwa na:

  • Sifa za kitaaluma zinazotakiwa kwa nafasi husika.
  • Uwezo wa kufundisha kwa ufanisi na kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya ualimu.
  • Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo ya mshahara wa kila mwezi, ingawa posho na motisha zinaweza kutolewa kulingana na taratibu zilizowekwa.

Mafunzo na Usimamizi

Walimu wa kujitolea wanapewa:

  • Mafunzo ya awali kabla ya kuanza kazi ili kuwaandaa kwa majukumu yao.
  • Mafunzo ya mara kwa mara ili kuboresha ujuzi na maarifa yao.
  • Usimamizi wa karibu kutoka kwa wakuu wa shule na maafisa elimu ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi na kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya ualimu.

Faida kwa Walimu Kujitolea

Walimu wanaojitolea wanapata:

  • Uzoefu wa kazi katika mazingira halisi ya shule.
  • Fursa ya kuonyesha uwezo wao na kujenga wasifu mzuri wa kazi.
  • Uwezekano wa kupewa kipaumbele katika ajira za kudumu zinazojitokeza.

Pakua PDF hapa ya walimu kujitolea na sifa za kuchukuliwa. au sikiliza hapa kutoka Bunge la Tanzania moja kwa moja.

Hitimisho

Mwongozo wa Walimu Kujitolea ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa walimu wanaojitolea wanatambuliwa, wanapewa mafunzo na usimamizi unaofaa, na wanapata fursa ya kuchangia katika maendeleo ya elimu nchini Tanzania. Kwa wale wanaopenda kujitolea kama walimu, mwongozo huu unatoa mwongozo wa wazi na wa haki wa jinsi ya kuhusika katika sekta ya elimu.

Kwa maelezo zaidi na kupata nakala ya mwongozo huu, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia:

Soma zaidi: Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal na Utumishi 2025 / 2026 PDF

1 Comment

  • Ni kwa kada za ualimu tuu? Vip kwa tunaojitolea kwenye taasisi mbali mbali za serikali? binafsi nina miaka 6 ktk idara ya maendeleo ya jamii kituo changu ni Moshi manispaa

Leave a Comment