Haya hapa Matokeo ya Usaili Ajira Portal Kada za Ualimu kwa Mwalimu daraja la IIIA Elimu ya awali, Kemia, daraja la III B Jiografia (Geograph), Tehama
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni taasisi ya serikali inayojitegemea, iliyoanzishwa mahsusi kurahisisha mchakato wa kuajiri watumishi katika Utumishi wa Umma. Sekretarieti hii ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).
Wasailiwa wote waliochaguliwa (SELECTED) wanatakiwa kuzingatia muda na eneo la usaili. Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates) Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na vitambulisho vyao.
- MWALIMU DARAJA LA III A – ELIMU YA AWALI
- MWALIMU DARAJA LA III B – JIOGRAFIA (GEOGRAPHY)
- MWALIMU DARAJA LA III B – TEHAMA (INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGY)
- MWALIMU DARAJA LA III B (BAIOLOJIA)
- MWALIMU DARAJA LA III B (KEMIA)
Dira
Kuwa Kituo Bora cha Uajiri katika Utumishi wa Umma katika kanda.
Dhamira
Kuhakikisha mchakato wa kuajiri watumishi wa umma unafanywa kwa kutumia mbinu za kisasa, huku ukizingatia usawa, uwazi, na sifa, pamoja na kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala yanayohusiana na ajira.
Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira
Jukumu kuu la PSRS ni kuratibu mchakato wa kuajiri katika Utumishi wa Umma. Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 ya mwaka 2002, kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1), majukumu ya Sekretarieti ni pamoja na:
- Kutafuta wataalamu wenye ujuzi maalum na kuandaa hifadhidata yao kwa ajili ya kuwarahisishia kuajiriwa.
- Kusajili wahitimu na wataalamu kwa ajili ya kurahisisha mchakato wa kujaza nafasi wazi za kazi.
- Kutangaza nafasi za kazi zilizopo kwenye Utumishi wa Umma.
- Kuwashirikisha wataalamu husika kwa ajili ya kufanya usaili.
- Kuwashauri waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uajiri.
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote yanayoelekezwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma.
Soma zaidi: