Jobs in Tanzania

Majina ya Walioitwa Kazini Ajira Portal “Utumishi”

Majina ya Walioitwa Kazini Ajira Portal "Utumishi"

Hii hapa orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Ajira Portal Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawapongeza waombaji wote waliofaulu usaili uliofanyika kati ya tarehe12-10-2024 na 15-04-2025. Matokeo ya usaili huo yameorodheshwa rasmi, na yanahusisha pia baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Hatua za Kuchukua kwa Waombaji Waliofaulu

  1. Kuchukua Barua za Kupangiwa Kazi:
    • Waombaji waliofaulu wanapaswa kuchukua barua zao za kupangiwa kituo cha kazi ndani ya siku saba (7) kutoka tarehe ya tangazo hili.
    • Barua zinapatikana katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira, zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya Wazi.
    • Ikiwa barua hazitachukuliwa ndani ya muda huo, zitatumwa kwa anuani za posta za wahusika.
  2. Kuripoti kwa Mwajiri:
    • Waliofaulu wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri wao kama ilivyoainishwa katika barua walizopangiwa.
    • Wakiwa kazini, wanapaswa kuwasilisha vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki.
  3. Vitambulisho Muhimu kwa Ajili ya Utambuzi:
    Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho miongoni mwa vifuatavyo:
    • Kitambulisho cha Uraia
    • Hati ya Kusafiria
    • Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
    • Kitambulisho cha Mpiga Kura
    • Leseni ya Udereva

Kwa Waombaji Wasiopata Nafasi

Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, tunapenda kuwahimiza kutokata tamaa. Endeleeni kufuatilia matangazo ya nafasi za kazi zitakapotangazwa tena na hakikisheni mnaomba kwa wakati.

Mwisho wa Taarifa

Tunawatakia kila la heri waombaji wote waliofaulu wanapoanza safari yao mpya ya ajira. Kwa maswali zaidi, tafadhali tembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira au wasiliana kupitia namba na anuani zilizotajwa kwenye tangazo rasmi.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma – Kazi kwa Weledi na Uadilifu.

Bonyeza hapa ku-download PDF

Soma zaidi:

Leave a Comment