Hii hapa Fomu ya Kujiunga Kidato cha Tano Florian 2025 joining instruction shule ya secondary Mkoani Arusha kwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule hiyo kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Ninafurahi kukuarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya sekondari Florian kwa mchepuo wa CBG/CBA/HGL.Kuchaguliwa kwake ni kutokana na kufanya vizuri katika mitihani yake ya kidato cha nne mwaka 2024.
Shule ya sekondari Florian iko katika kijiji cha Endamarariek,wilaya ya Karatu-mkoa wa Arusha Km 21 kutoka Karatu mjini kando ya barabara ya Karatu kwenda Mbulu.
Shule ipo katika mazingira mazuri na hali ya hewa nzuri ya mwanafunzi kusoma na kujisomea. Kutoka Arusha mjini mpaka Karatu mjini nauli ni kati ya Tsh 5000 kwa mabasi na Hiace na Tsh 7,000 kwa usafiri wa Noah. Ila usafiri wa Noah ni wa haraka zaidi. Kwa wanaotoka mikoa ya Mara na simiyu wanaweza kutumia magari yanayopita Serengeti na watashukia Karatu Mjini. Na wanaotokea Babati, Singida na Dodoma wanaweza kushukia Makuyuni na kupanda magari yanayokwenda Karatu mjini. Upo usafiri wa Dar-es-salaam hadi karatu kwa kutumia mabasi ya Dar express na Saibaba. Nauli kutoka Karatu mjini mpaka Florian sekondari ni Tsh 2,000 hadi 3,000 Ukitokea Mbulu nauli ni Tsh 5,000 hadi kituo kinachofahamika kwa jina la Kibaoni, kutoka kibaoni haadi shuleni unaweza kutembea au kutumia usafiri wa bodaboda kwa gharama ya Tsh 1000/= tu .
Ofisi ya Rais TAMISEMI ni Wizara pekee ambayo Makao Makuu yake yalianzia Jijini Dodoma tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini tangu Serikali ilipotangaza Makao Makuu ya Serikali kuwa ni Dodoma na kwa Dar es salaam kumekuwa na Ofisi ndogo. Uwepo wa Makao Makuu Dodoma ulikua na lengo la kutoa fursa sawa kwa wadau wake wakuu hususan Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufika Dodoma kwa urahisi wanapofuata huduma mbalimbali.
Dhima
Kutengeneza mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma, Maendeleo Vijijini na Mijini, Sheria, Miongozo na Viwango ili kuiwezesha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa huduma bora kwa wananchi na kuondoa umaskini.
Pakua PDF hapo chini yenye maelezo kwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2025.
GIPHY App Key not set. Please check settings