Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amepata Kibali cha Ajira Mpya chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 chenye nafasi ya Dereva Daraja la II (8) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Tandahimba anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuomba maombi ya nafasi za kazi zifuatazo:
Nafasi: Dereva Daraja II – Nafasi 8
Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Muda wa Maombi: 04 Juni 2025 hadi 18 Juni 2025
Muhtasari wa Kazi: Hakuna
Majukumu ya Kazi:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake
Sifa za Mwombaji:
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha Nne na leseni ya daraja E au C ya uendeshaji magari, ambayo ameitumia kwa kazi kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehitimu mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi kutoka VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara: Ngazi ya TGS B kwa mujibu wa viwango vya Serikali
Tuma maombi hapa.
GIPHY App Key not set. Please check settings