Ajira Mpya za Walimu 2025 Nafasi 1714 MDAs & LGAs Ajira portal ualimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha Maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi (10) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Nafasi: Mwalimu III B, C – Nafasi 1714
Mwajiri: Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs)
Muda wa Kutuma Maombi: 05 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025
Majukumu ya Mwalimu
- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
- Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
- Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
- Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
- Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
- Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
- Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
Sifa za Mwombaji
1. Mwalimu Daraja la III C Fizikia
- Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fizikia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Fizikia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
2. Mwalimu Daraja la III C Somo la Biashara
- Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Biashara au Usimamizi wa Biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration)
- AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biashara au usimamizi wa biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
- AU Wenye Shahada isiyo ya Ualimu katika fani ya Biashara/usimamizi wa biashara/Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration/Business studies’’. waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.
3. Mwalimu Daraja la III B Somo la Food Production
- Kuajiriwa mwenye cheti cha mafunzo ya Stashahada ya Ualimu yenye somo la kufundishia la Uzlishaji chakula (Food production/ Culinary Arts) kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
- AU Wenye Stashahada isiyo ya Ualimu katika fani ya Huduma ya Chakula, vinywaji na mauzo (Food production/ Culinary Arts). Waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.
4. Mwalimu Draja la III C Somo la Nishati
- Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye la Somo la Ufungaji wa Nishati ya Jua (Solar Power Installation au ‘’Power and Renewable Energy engineering’) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Somo la Ufungaji wa Nishati ya Jua (Solar Power Installation au ‘’Power and Renewable Energy engineering’’). Pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
- AU Wenye Shahada isiyo ya Ualimu katika fani ya somo la kufundishia la Somo la Ufungaji wa Nishati ya Jua (Solar Power Installation au ‘’Power and Renewable Energy engineering’’). Waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.
5. Mwalimu Daraja la III B Somo la Ushonaji
- Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la ushonsji au “Home Economics” kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
- AU Wenye Stashahada isiyo ya Ualimu katika fani ya ushonaji au ‘’Home economicas’’. waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.
6. Mwalimu Daraja la III B Somo la Huduma ya Chakula
- Kuajiriwamwenyechetichamafunzo ya StashahadayaUalimuyenyesomolakufundishialaChakulana vinywaji, mauzo na huduma “Foodandbevarage, sales and services”kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
- AUWenyeStashahadaisiyoyaUalimukatikafaniyaHudumayaChakula,vinywaji na mauzo “Food and bevarage, sales and services”. Waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.
7. Mwalimu Daraja la III C Somo la Uchumi
- Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Uchumi (Economics)
- AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Uchumi (Economics) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
Jinsi ya kutuma maombi
Bonyeza hapo chini kupakua PDF.