Action For Ocean (AFO) wanatafuta Finance Manager mwenye uzoefu kujiunga na timu ya uongozi (Senior Management Team) jijini Dar es Salaam. Hii ni nafasi ya kiuongozi yenye jukumu la kusimamia mikakati ya kifedha, ufuatiliaji wa masharti ya wafadhili, na kusaidia ukuaji wa taasisi tunapopanua athari zetu katika maeneo ya pwani ya Tanzania.
Ikiwa wewe ni CPA/ACCA na una uzoefu wa zaidi ya miaka 5 katika masuala ya fedha za NGO, na unatamani kuchangia kwenye ujenzi wa blue economy yenye nguvu na ustahimilivu—nafasi hii ni yako.
Mahali: Dar es Salaam (na safari za mara kwa mara za kikazi)
Mwisho wa kutuma maombi: 14 Septemba 2025 (maombi yanapitiwa kadri yanavyopokelewa)
Tunawahimiza kwa dhati wanawake na waombaji kutoka jamii za pwani kuwasilisha maombi.