Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anawataarifu waombaji wote wa ajira kuwa usaili wa kazi utafanyika kuanzia 15 Septemba 2025 hadi 18 Septemba 2025. Waombaji wote walioitwa wanatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwa muda na sehemu iliyoainishwa kwa kada husika.
- Ni lazima kuvaa barakoa (mask) na kuwa na kitambulisho halali: NIDA, kura, uraia, kazi au hati ya kusafiria.
- Wasilisha vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, kidato cha VI, Astashahada na Diploma.
- Dereva wanatakiwa kuwa na leseni halali na cheti kutoka NIT au chuo kinachotambulika.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na results slips hazitakubaliwa.
- Waombaji waliomaliza nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NACTE au NECTA.
- Kwa wasailiwa wenye tofauti ya majina, leta Affidavit au Deed Poll.
- Msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Hakikisha umenakili namba ya mtihani kupitia akaunti yako kwani hazitatolewa siku ya usaili.
- Waombaji wasiokuwa kwenye orodha ya wasailiwa watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
Kwa majina ya walioitwa kwenye usaili na maelekezo zaidi, tembelea tovuti ya Halmashauri ya Temeke au ofisi ya utumishi.