Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Kagera PDF Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga pamoja na shule walizopangiwa kwa mwaka wa masomo 2025. Uchaguzi huu umezingatia matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka 2024, pamoja na vigezo vya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023).
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa
Wazazi, walezi na wanafunzi wanaweza kuangalia majina kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI kwa kutumia kiungo maalum:
Bonyeza hapa kuangalia waliochaguliwa Form Five Mkoa wa Kagera
Unaweza pia kusikiliza hotuba ya Waziri akitangaza majina ya waliochaguliwa kidato cha tano na kujiunga na vyuo vya kati kupitia viunganishi vilivyopo kwenye tovuti hiyo tafta zaidi hapa Fursa za Ajira Tanzania.
Idadi ya Wanafunzi Waliochaguliwa
Taarifa ya TAMISEMI inaonyesha kuwa:
- Wanafunzi 149,818 (sawa na 69.96%) wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano.
- Wanafunzi 64,323 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu.
- Jumla ya wanafunzi 214,141 walikidhi sifa, wakiwemo:
- Wasichana: 97,517
- Wavulana: 116,624
- Wenye mahitaji maalumu: 1,028
Kupitia Kiungo cha TAMISEMI Unaweza:
- Kutafuta jina kwa kutumia namba ya mtihani (Index Number).
- Kuona shule aliyopangiwa mwanafunzi.
- Kupata maelekezo ya kujiunga na shule husika.
Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Waliochaguliwa
Wanafunzi wanapaswa:
- Kupakua barua za mwaliko na fomu za kujiunga (Joining Instructions) kupitia tovuti ya TAMISEMI au shule husika.
- Kusoma kwa makini maelezo ya barua hizo, ikiwemo tarehe ya kuripoti, mahitaji ya shule na ada (ikiwa ipo).
- Kuwasiliana na shule moja kwa moja kwa maswali au ufafanuzi zaidi.
Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025
TAMISEMI inawapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa. Inawahimiza kujiandaa vyema kwa safari mpya ya elimu ya sekondari ya juu. Kwa walioikosa nafasi, wanashauriwa kufuatilia awamu zinazofuata au kuwasiliana na ofisi za elimu za mikoa na wilaya.
Mawasiliano ya TAMISEMI
- Barua pepe: ps@tamisemi.go.tz
- Simu: +255 262 321 234
- Tovuti rasmi: www.tamisemi.go.tz
GIPHY App Key not set. Please check settings