Haya hapa matokeo ya usaili wa Vitendo uliofanyika tarehe 04/06/2025 Ajira portal Wasailiwa wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia muda na eneo la kufanyia usaili. Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates) pamoja na kitambulisho.
Dhamira
Kufanya mchakato wa ajira kwa Watumishi wa Umma kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kuzingatia misingi ya usawa, uwazi, na sifa, pamoja na kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala yanayohusiana na ajira.
Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Jukumu kuu la Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni kurahisisha ajira katika Utumishi wa Umma. Kulingana na Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu cha 29(1), majukumu ya PSRS ni kama ifuatavyo:
- Kusaka wataalamu mbalimbali wenye ujuzi maalum na kuandaa hifadhidata ya wataalamu hao ili kurahisisha ajira;
- Kusajili wahitimu na wataalamu kwa ajili ya kumbukumbu na urahisi wa kujaza nafasi wazi;
- Kutangaza nafasi wazi za kazi zinazojitokeza katika utumishi wa umma;
- Kuwatumia wataalamu stahiki kwa ajili ya kufanya usaili;
- Kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na ajira; na
- Kufanya jambo au kitendo kingine chochote kitakachoelekezwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma.
Maadili ya Msingi
Maadili ya msingi ya PSRS ni nguzo muhimu za utendaji kazi na mwenendo katika kukabiliana na mabadiliko ya kijamii, kiserikali, kisiasa na kiteknolojia. Maadili hayo ni kama yafuatayo:
- Ufuatiliaji wa ubora katika utoaji huduma;
- Uaminifu kwa Serikali;
- Bidii katika kazi;
- Uadilifu;
- Ukarimu kwa wote;
- Kuheshimu sheria; na
- Matumizi sahihi ya taarifa za serikali.
Pakua PDF hapo chini.
GIPHY App Key not set. Please check settings